



KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, leo imeingia mitaani kuzungumza na wateja wake kuhusiana na ofa kabambe ijulikanayo kama ‘HATUPIMI Bando’ inayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
Airtel HATUPIMI Bando inapatikana katika vifurushi mbalimbali kikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisizo na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi.
Akizungumza na wanahabari wakati wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Airtel wakitembelea wateja wake wa jiji la Dar es Salaam kujua na kuwaelekeza namna ofa hiyo inavyopatikana na namna na kujiunga, Meneja Biashara wa Kanda wa Airtel, Robert Sanyagi alisema: “Tunatembelea wateja wetu wa mkoa wa Dar es Salaam ili kuingiza rasmi huduma nafuu kwa kuwa wanaamini katika kuendelea kuboresha huduma zao ili kukidhi mahitaji ya wateja na ili mteja kila anapomuona mtoa huduma wa Airtel apate msaada juu ya ofa hiyo ya ‘HATUPIMI Bando’.
“HATUPIMI Bando itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau mbalimbali kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua kikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali kumalizika kabla ya wakati.
“Kuna vifurushi vya HATUPIMI kwa siku vya hadi Sh 1,000 pia vipo vya wiki kwa Sh 5,000 na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa Sh 10,000, ili ufurahie huduma ya kutopimiwa dakika zako na uongee bila kikomo.”
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano, alifafanua kuwa ili kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando, mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# kisha kuchagua 1 kupata HATUPIMI kisha anachagua bando ya siku, wiki au mwezi kulingana na mahitaji yake.
“Airtel tunaamini ofa hii ni ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru wa kuongea watakavyo bila kikomo,”alisema Singano.
Na Denis Mtima/GPL