The House of Favourite Newspapers

Upungufu wa Nguvu za Kiume; Sababu na Tiba

Na Daktari wa Amani| Gazeti la Amani| Makala

WIKI iliyopita tulianza kuangalia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na tuliangalia utangulizi wa mada hii, leo ningependa kuendelea na vyanzo vinavyosababisha tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazosababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa walio wengi:

KUFANYA PUNYETO KWA MUDA MREFU

Mtu anapopiga punyeto anakuwa anaiminya mishipa inayosababisha kusimama kwa uume, baada ya muda fulani, mishipa hiyo huishiwa nguvu na kulegea na hivyo linapokuja suala la kusimamisha uume, mwanaume huyu anakuwa hana uwezo tena.

MATUMIZI YA MARA KWA MARA YA MADAWA MAKALI YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME (HASA MADAWA YA KIZUNGU)

Madawa haya husababisha mishipa ya uume kulegea kwa sababu hui-overdose mishipa hiyo na kuilazimisha kufanya kazi zaidi ya kiwango chake. Matumizi haya yanapokuwa ya muda mrefu humfanya mhusika kuwa tegemezi na pia hufanya mishipa ya uume wa mhusika kulegea na kukosa nguvu.

ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA KWA WINGI

Kwa sababu huathiri moyo na mzunguko wa damu mwilini na hivyo uume kukosa msukumo wa damu wa kutosha katika mishipa yake ya damu.

PRESHA NA UGONJWA WA KISUKARI

Uoga au wasiwasiwa kufanya tendo la ndoa kutokana na kutokujiamini.

ULEVI KUPITA KIASI

Mfano ulevi kupita kiasi wa pombe, madawa ya kulevya husababisha mwanaume kupoteza nguvu za kiume. Msomaji ningependa kukujulisha kuwa tafiti zinaonesha unywaji pombe unaathari nyingi katika afya ya binadamu, husababisha tatizo la kuharibika kwa ini (liver damage), uharibifu wa mfumo wa fahamu (nervous system) na kuvuruga mpangilio wa uzalishaji wa homoni (kichocheo) ya uzazi ya kiume na hatimaye kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

MSONGO WA MAWAZO AU UCHOVU KUPITA KIASI

Hii husababisha mwanaume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa katika sita kwa sita na mke wake. Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango cha kutosha cha vichocheo vya kufanya tendo la ndoa.

Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazima tezi dume lake liwe na afya bora. Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage, vitunguu, matango, karoti, spinachi, kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.

Zipo sababu nyingine nyingi zinazosababisha tatizo hili kama vile magonjwa kama ngiri na kupooza kwa mwili. Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu. Tukutane wiki ijayo.

Comments are closed.