×

Global Yatoa Nailoni za Mvua kwa Wauza Magazeti Dar

KAMPUNI ya Global Publishers wachapaji wa Magazeti ya Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi na Championi leo imetoa nailoni za kujizuia mvua kwa wauzaji wa magazeti wa viunga mbalimbali vya Jiji la Dar.

Nailoni hizo zimesambazwa kwa udhamini wa British School ya Mwenge jijini Dar kupitia mwakilishi wake, Sekunda Pius na Ofisa Utawala wa Global Publishers, SoudyKivea kwa kuzunguka na kugawa kwa baadhi ya wauzaji wa viunga vya Jiji la Dar ikiwemo Tegeta, Kunduchi, Kariakoo, Posta, Ubungo na kwingine kwa ajili ya kuzuia kulowanisha magazeti kipindi cha mvua.   

…akiwapatia nailoni wauzaji wa Ubungo, Dar.

Mwakilishi wa British School ya Mwenge jijini Dar na Ofisa Tawala wa Global Publishers, Soudy Kivea wakimpatia nailoni ya kufunikia magazeti, muuzaji wa Mwenge, mama mchungaji.

Wawakilishi wa Global wakitoa nailoni kwa wauza magazeti wa Posta jijini Dar.

Kivea akiwapatia nailoni mavenda wa Mwenge.
Muuzaji wa Gerezani, Kariakoo akisaidiwa na Kivea kufunika magazeti.
Muuza magazeti wa Kunduchi jijini Dar, Chris akisaidiwa kufunika magazeti na Kivea baada ya kupewa nailoni la kuzuia magazeti kulowana.
Muuzaji wa Kigogo Mwisho, Samweli Shikuni akifunika magazeti kuzuia mvua.
Kivea akimfunikia muuza magazeti wa Tegeta kwa Ndevu, Badilu Mahere.

Wauzaji wa Kariakoo, Dar wakipewa nailoni za kufunikia magazeti wakati wa mvua.
…akiendelea kugawa nailoni kwa wauzaji wa Tegeta.

Na mwandishi wetu/GPL