
Msafara wa wachezaji wa Yanga ambao ulichelewa ndege nchini Algeria, unatarajiwa kuwasili mchana wa leo baada ya kukamilika kwa masuala ya kubadilisha tiketi.
Yanga ilitupwa nje katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-1 kutoka kwa MC Alger ya Algeria, lakini wakati wa kuondoka kutoka nchini humo, walikuwa na ratiba ya kurejea nchini kimafungu, kundi la kwanza lilifanikiwa kuondoka salama.

Kundi la pili halikuwezekana kuondoka baada ya kuelezwa kuwa walichelewa ndege. Waliochelewa ndege ni wachezaji 11 wakiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa.
Walioachwa waliokuwa waondoke nchi Algeria, juzi Jumapili kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.
Taarifa kutoka Yanga zinaeleza kuwa walifanikiwa kufanya mabadiliko na sasa watawasili mchana wa leo Jumanne, ambapo Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) lilisaidia kufanikisha mchakato huo.