The House of Favourite Newspapers

Babu Ally Aitaka TFF Kuacha Ubabaishaji

0
Kutoka kushoto ni mchambuzi wa soka na muongoza kipindi cha Spoti Hausi, Saleh Ally, Philip Nkini, Babu Ally, Kassim na Wilbert Molandi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kupindi.

Shabiki mkubwa wa timu ya soka ya Kauzi ya Tandika jijini Dar es Salaam, Ally Mussa Nalyamba ‘Babu Ally’ akieleza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuacha ubabaishaji katika suala zima la uendeshaji wa soka hapa nchini.
Saleh Ally akifunga kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na  Global TV Online kila siku ya Alhamisi saa kumi kamili jioni.

SHABIKI mkubwa wa timu ya soka ya Kauzi  ya Tandika jijini Dar es Salaam, Ally Mussa Nalyamba ‘Babu Ally amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuacha ubabaishaji katika suala zima la uendeshaji wa soka hapa nchini.

Babu Ally ambaye ni mlemavu wa macho (haoni) lakini amekuwa akifuatilia kwa kalibu kabisa michuano ya  Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za timu ya za taifa ameyasema hayo leo alipokuwa kuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha michezo cha Spoti Hausi kinachorushwa na TV ya mtandaoni ya Global TV Online.

Leave A Reply