×

Mjema Atembelea Soko la Buguruni, Achukizwa Uuzaji Bidhaa Chini

DC Mjema akikagua soko la Buguruni.
…Akipata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa soko hilo.

Stori: Denis Mtima na Hilaly Daudi.

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema leo ametembelea soko la Buguruni jijini Dar es Salaam kukagua  miundombinu ya soko hilo ambapo pia alichukizwa na baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo wanaoweka bidhaa zao chini hatua aliyoisema inaweza kusababisha kipindupindu na magonjwa ya mlipuko.

Akizungumza wakati akiwa sokoni hapo Mjema alisema kuwa lengo lake la kutembelea soko hilo ni kuona miundombinu ya soko na kukagua ujenzi unaoendelea kama inaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao pasipokuwa na adha yoyote.

“Wafanyabiashara wa soko hili wanapaswa kuzingatia usafi wa mazingira yao wanayofanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuondoa uchafu wa bidhaa zilizoharibika ili kuweka mazingira safi ya kufanyia kazi,” alisema.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alijionea bidhaa mbalimbali na bei zake zinazouzwa sokoni hapo, hali iliyomvutia.

Leave a Comment