×

ARUSHA: Watano Wafariki Dunia Baada ya Nyumba Kuangukiwa na Mti

ARUSHA: Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na mti katika eno la Sokoni Two, Kijiji cha Kinyeresi, wilayani Arumeru, Arusha,  usiku wa kuamkia leo.

Tukio hilo limetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kila kona ya nchi ambapo mti huo uling’olewa na mvua hizo kisha kuiangukia nyumba na kusababisha maafa hayo.

Mashuhuda wamesema waliofariki dunia ni vijana kati ya miaka 11-31  miongoni mwao wakiwa  wanafunzi.


Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi!

 

Leave a Comment