×

AJALI: Basi la Allys na Coaster Yagongana Shinyanga, 60 Wanusurika Vifo

SHINYANGA: Watu zaidi ya 60 wamenusurika kifo, huku 26 kati yao wakijeruhiwa vibaya baada ya basi mali ya Kampuni ya la Allys na basi dogo aina ya Coaster kugongana uso kwa uso mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Kizumbi, Mbuyuni ambapo inasemekana mabasi hayo yamegongana kwenye kona.
Basi la Allys lilikuwa likisafiri kutoka Mwanza liligongana na Coaster inayofanya safari kati ya Isanzu na Kahama.
Credit -ITV
Endelea kufuatilia taarifa zetu tutakujuza zaidi.

Leave a Comment