

BAADHI ya Watanzania wamekuwa wakikwama kuendeleza miradi yao kutokana na kukosekana kwa wataalam wenye taaluma ya kuratibu miradi hiyo.
Hayo yamesemwa jijini Dar na Mkurugenzi wa Chuo cha Usimamizi wa Miradi (TIPM), Lwitiko Mwalukasa, alipokuwa akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam.
Alifafanua kuwa miradi mingi imekwama ama kutokamilika kwa muda mrefu kwa kuwa watu wanaowachagua kuratibu miradi hiyo hawana taaluma hiyo.
Alisisitiza kuwa sasa taasisi yake inazo fursa kwa watu mbalimbali kufika hapo katika jengo la Investment House (Kitegauchumi) eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
Na Denis Mtima | GPL