×

Askofu Gadi Aomboleza Vifo vya Wanafunzi 32

ASKOFU wa Kanisa la Good News For All Ministry la jijini Dar es Salaam, Dkt. Charles Gadi ameomboleza vifo vya wanafunzi 32, walimu wao wawili na dereva vilivyotokea Jumamosi iliyopita wilayani Karatu mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Dkt. Gadi alisema kuwa kanisa lake linashirikiana na serikali na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuomboleza vifo vya watoto hao.

Kutoka kushoto ni mchungaji Andrew Thomas, Askofu Dkt. Charles Gadi (katikati) na Mchungaji Palemo Masawe ambaye ni katibu mkuu wa Good News For All Ministry.

Dkt. Gadi alisema kuwa huo ni msiba mkubwa na wa kusikitisha kwa taifa ulioacha pengo kubwa kwa wanafamilia hivyo anaomba Mungu awajalie fafaja ya Roho Mtakatifu kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.

“Tunaipongeza serikali yetu ya awamu ya tano kupitia kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa jinsi ilivyochukulia msiba huu kwa uzito mkubwa, jambo ambalo limewaunganisha  Watanzania kuwa kitu kimoja katika maombolezo haya” alisema.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

VIDEO: Mama wa Mtoto Aliyenusurika kwa Mabomu Akafariki kwa Ajali Karatu

Leave a Comment