×

IYF Yatoa Elimu ya Maadili ya Wanafunzi kwa Walimu

Mkurugenzi wa IYF hapa nchini, Jeon Hee Yong akizungumza na wanahabari.

Mkurugenzi Msaidizi wa IYF, Levin Ndengerio naye akifafanua jambo.

Mmoja wa walimu kutoka Shule ya Sekondari Mbweni, Christian Mjawa aliyehudhuria kongamano hilo akielezea alivyofaidika na kongamano hilo.

 Baadhi ya wahudhuriaji waliofika katika kongamano hilo.

Taasisi ya International Youth Fellowship (IYF), imetoa elimu juu ya maadili mema ya wanafunzi wao kwa baadhi ya walimu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari leo, Mkurugenzi wa IYF hapa nchini, Jeon Hee Yong alisema kuwa kongamano hilo lilikuwa la siku tatu na lilikutanisha vijana mbalimbali pamoja na walimu ili kuweza kupata elimu inayohusu umuhimu wa vijana kujitambua na kujithamini wao wenyewe.

Baadhi ya vijana raia wa Wakorea wakitoa burudani.

Alisema kuwa kwa hakika walimu waliohudhuria kongamano hilo watafikisha elimu waliyoipata kwa walimu wao ili nao waweze kuwa na maadili mema katika kizazi kijacho.

Alifafanua kuwa IYF ilianzia Korea ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana, kujiamini na kuweza kufanya shughuli zao vizuri katika kupambana na maisha.

..Wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kikiendelea.

“Hivi sasa IYF ina matawi zaidi ya 80 duniani na lengo letu ni kutoa elimu kwa vijana kuhusu namna ya kupambana na maisha,” alisema Hee Yong.
NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment