×

TANZIA: Sozigwa na Mwambungu Wafariki Dunia Muhimbili

#TANZIA: Tanzania imepata misiba miwili baada ya kuondokewa na watu wawili ambao waliwahi kushika nyadhifa za juu kwenye uongozi wa awamu zilizopita.

Viongozi hao ni aliyewahi kuwa mwandishi wa habari wa Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Paul Sozigwa ambaye amefariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taratibu za msiba wa Mzee Paul Sozigwa zinafanyika nyumbani kwa mtoto wake, Lucy, Mtoni Mtongani baada ya round about karibu na kanisa la KKT ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu, nyumbani kwao Kisarawe, Pwani.

Mwingine ni aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu ambaye amefariki dunia katika taasisi hiyohiyo ya Moyo ya Jakaya Kikwete, ambako alikuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Mwenyezi Mungu azilaze Mahali Pema Peponi Roho za Marehemu, Amina!

Leave a Comment