



Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki (IITA) leo imeadhimisha na wanafunzi Siku ya Umuhimu wa Mimea Duniani kwa kusherehekea kwenye maabara maalum na watoto wa shule ili waweze kujifunza masomo ya kisayansi kwa bidii.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa IITA , Victor Manyong amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utafiti wa kilimo ili kuwasaidia wakulima katika mchakato wa kilimo na ndiyo maana siku hii hushirikisha watoto ambao ni vyema wakipata mafunzo tangu awali ili kufikia mafanikio ya kisayansi.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwakabili wakulima kwa kukosa vitendea kazi vya kisasa pamoja na upungufu wa pembejeo na mbegu.
Maadhimisho ya Siku ya Umuhimu wa Mimea Duniani huadhimishwa Mei 18, kila mwaka.
Na Denis Mtima/GPL