×

Sirro Atoa Kauli Sakata la RC Dar Kuvamia Clouds Media

Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, akizungumza na wanahabari leo.

DAR ES SALAAM: Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro,  amesema uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha radio na televisheni cha Clouds bado unaendelea.

Kamanda Sirro aliyasema hayo leo ofisini kwake baada ya kubanwa na wanahabari.

“Nawaomba watu wa Clouds, watoe ushirikiano kwa wapelelezi wangu ili shauri hilo lihame kwenye ofisi yangu na kulipeleka ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka) kwa hatua zaidi,” alisema Kamanda Sirro.

 

Video: Sirro Atoa Kauli Sakata la RC Dar Kuvamia Clouds Media

Leave a Comment