The House of Favourite Newspapers

Video: Kauli ya Kwanza ya IGP Simon Sirro Baada ya Kuapishwa

0

IKULU, DAR ES SALAAM: Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Nyakoro Sirro amesema kuwa lengo lake kubwa baada ya kukabidhiwa wadhifa huo mpya ni kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua na anaimani kubwa kuwa atafanikiwa kwa sababu wananchi ambao ni wema ni wengi kuliko wahalifu.

Simon Sirro ameyasema hayo leo mara tu baada ya kupandishwa cheo na kuwa Inspeka Jenerali wa Jeshi la Polisi na kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, IGP Sirro amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ili wafanikiwe kutokomeza uhalifu kwa sababu wahalifu wanaishi ndani ya jamii, hivyo Polisi peke yao hawatafanikiwa.

“Ombi langu kwa Watanzania, ili tuweze kuishi kwa amani na utulivu, ni vizuri sana wakatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. Naamini kabisa tutaweza kwa sababu hawa wahalifu ni wachache na sisi ni wengi, kwa hiyo umoja wetu ule ni lazima tutashinda” amesema IGP Sirro wakati akihojiwa na maafisa wa habari wa Ikulu.

Mbali na kuomba ushirikiano huo kwa raia, IGP Sirro ametoa onyo kwa wahalifu kuwa, siku zote uhalifu haulipi, na ukiung’ang’ania sana, utasababisha ukaiacha kazi yako.

Msikilize hapa chini IGP Sirro akizungumza;

 

Leave A Reply