×

VIDEO: Mwili wa Mchora Nembo ya Taifa Ulivyoagwa na Kusafirishwa

Mzee Francis Maige, enzi za uhai wake.

Na Elvan Stambuli

Mwili wa Francis Maige ‘Ngosha” anayedaiwa kuchora ngao ya taifa, umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kusafirishwa kupelekwa  nyumbani kwao kijijini Bulima, Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza kwa mazishi.

Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) akizungumza na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza (kulia) na katikati ni Mwakilishi wa Shirikisho la Sanaa na Ufundi, Adrian Nyangamale.

Katika shughuli za kuaga mwili wa mzee Ngosha, watu mbalimbali walihudhuria wakiongozwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii na Watoto,Marcel Katemba, wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata), Godfrey Mungereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, madaktari akiwemo daktari aliyekuwa akimuhudumia marehemu Dk. Mfinanga, pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharula Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akielezea ugonjwa, tiba na kifo cha Mzee Maige.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, mzee Ngosha alifariki dunia baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa anapatiwa matibabu ambapo leo Dk Mfinanga alisema chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa kifua kikuu ambao ulimsumbua kwa muda mrefu na ulichangiwa na ukosefu wa lishe bora mwilini.

Mwili wa marehemu Ngosha unatarajiwa kuzikwa kesho kijijini Bulima, Misungwi, Mwanza.

Bwana Karim Mahmoud Malapa ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malapa, Buguruni alikokuwa akiishi mzee Maige.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Marcel Katemba akimzungumzia Marehemu Mzee Maige.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mzee Maige.

Muombolezaji akilia kwa uchungu wakati wa kumuuaga marehemu.

Shigongo akiwaongoza waombolezaji wengine kuupeleka kwenye gari mwili wa marehemu kwa ajili yakusafirishwa kuelekea Misungwi kwa mazishi.

 

Mwili ukiiingizwa kwenye gari.

 

Safariu ya kuusafirisha mwili wa marehemu Mzee Maige ukisafirisha kwenda nyumbani kwao, Kijiji cha Bulima Wialaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi ikianza.

Muombolezaji akiwa na Nembo ya Taifa aliyoitengeneza kwa ajili ya kumuenzi Mzee Maige.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA

Leave a Comment