
Na Elvan Stambuli
Mwili wa Francis Maige ‘Ngosha” anayedaiwa kuchora ngao ya taifa, umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao kijijini Bulima, Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza kwa mazishi.

Katika shughuli za kuaga mwili wa mzee Ngosha, watu mbalimbali walihudhuria wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii na Watoto,Marcel Katemba, wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata), Godfrey Mungereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, madaktari akiwemo daktari aliyekuwa akimuhudumia marehemu Dk. Mfinanga, pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, mzee Ngosha alifariki dunia baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa anapatiwa matibabu ambapo leo Dk Mfinanga alisema chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa kifua kikuu ambao ulimsumbua kwa muda mrefu na ulichangiwa na ukosefu wa lishe bora mwilini.

Mwili wa marehemu Ngosha unatarajiwa kuzikwa kesho kijijini Bulima, Misungwi, Mwanza.




Muombolezaji akilia kwa uchungu wakati wa kumuuaga marehemu.

Shigongo akiwaongoza waombolezaji wengine kuupeleka kwenye gari mwili wa marehemu kwa ajili yakusafirishwa kuelekea Misungwi kwa mazishi.


Mwili ukiiingizwa kwenye gari.



Muombolezaji akiwa na Nembo ya Taifa aliyoitengeneza kwa ajili ya kumuenzi Mzee Maige.