The House of Favourite Newspapers

Azam Bado Watatu Tu Mziki Utimie

0

BAADA ya kufanya usajili wa nguvu kwa kuwanasa Mbaraka Yusuph na Salmin Hoza, Azam FC imesema imebakiza nafasi tatu za usajili ambazo ni beki mmoja, kiungo na kiungo mshambuliaji.

Azam ilimnasa Mbaraka kutoka Kagera Sugar baada ya Yanga kuchemka katika makubaliano na straika huyo kama ilivyokuwa kwa kiungo Hoza aliyetokea Mbao FC ya Mwanza. Ukiachana na Mbaraka na Hoza, Azam ilipandisha wachezaji watano kutoka timu yao ya vijana ambao wameiva kucheza msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Meneja wa Azam, Philip Alando ameliambia Championi Jumamosi kwamba, wamebakiza nafasi tatu katika timu yao ili kukamilisha usajili wao na tayari kuna wachezaji wanafanya nao mazungumzo.

“Bado tunaendelea na mchakato wetu wa usajili, kuna nafasi tatu zimebakia hadi sasa ili kukamilisha usajili na tayari kuna wachezaji tunafanya nao mazungumzo. “Tunahitaji kufanya mabadiliko katika kikosi chetu kwa kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara kwa kusajili wachezaji wenye vigezo,” alisema Alando.

KHADIJA MNGWAI | CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply