×

CCM Walaani Matamshi ya Lowassa… Waitaka Serikali Imchukulie Hatua

Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kauli za kichochezi na za kidini zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa nchini, zenye lengo la kuwafitinisha Watanzania.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduz, (CCM), Humphrey Polepole amebainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Alhamis Julai 29,  huku akiiomba serikali ikithibitika mtu amekosea serikali isiwe na ajizi kuchukua hatua kwa aina ya mtu huyo. Aidha, Polepole ameunga mkono kauli ya Rais Mstaafu Mzee Mwinyi, aliyoitoa hivi karibuni jijini Dar, kuwa anngependa Rais Magufuli kuona anaendelea kuongozo nchi hata baada ya muda wake kisheria kuisha.

Wakati pole pole akiyasema hayo,  leo tena aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amehojiwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi aliyoyatoa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati alipohudhuria futari iliyoandaliwa na Mhe, Waitara.
Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Katika hatua nyingine, Polepole amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaunga Mkono Kauli ya Rais Magufuli ya kutorudi masomoni kwa wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shule kwenye mfumo rasmi wa Elimu.

Polepole amesema kuwa wanafunzi waliopata ujauzito hawataweza kurudi shuleni kwenye mfumo rasmi isipokuwa kwenye Mfumo wa elimu ya watu wazima.

Leave a Comment