
TIB Group ina mashirika matatu yaliyoundwa kimkakati ili kuiwezesha serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi. Mashirika hayo ni
- TIB Development Bank Limited
- TIB Corporate Bank Limited
- TIB Rasilimali Limited
Pamoja na umoja huu, mashirika haya yanajitegemea kiundeshaji na utendaji, kila moja likisimamiwa na kuongozwa na dira na dhamira yake chini ya uongozi na bodi zao nazote zikiwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
TIB Group tunakukaribisha kutembelea banda letu la sabasaba ili upate elimu na taarifa mbali mbali kuhusu huduma zetu.
Taasisi zetu zinatoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwamo ushauri katika masuala ya mitaji na uwekezaji, mikopo ya miradi ya kimaendeleo na miundo mbinu pamoja na huduma mbalimbali za kibenki za biashara.
UWEZO TUNAO……Tumejipanga kutoa huduma mbali mbali za kifedha ili kusaidia ukuwaji wa biashara katika kuwezesha maendeleo ya viwanda.

TIB Development Bank Ltd (TIB DFI) ni Benki ya maendeleo inayojihusisha na kutoa mikopo mbali mbali ya muda wa kati na muda mrefu. Mikopo hii inalenga sekta muhimu zinazochochea maendeleo ya nchi. Sekta hizo ni pamoja na miundo mbinu, uanzishwaji na uundwaji wa viwanda mbalimbali, miradi ya Gesi, ufuaji wa madini, miradi ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo na miradi ya huduma za kijamii.
Uzoefu wa benki hii katika kuwezesha maeneo haya una msingi imara kutoka kuanzishwa kwa Taasisi hii mwaka 1970.
Kwa mawasiliano zaidi:www.tib.co.tz
TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi 6 kwa sasa, Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.
Benki inatoa huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki. Pia huduma ya ‘Premier Banking’ kwa wale wateja wanaopenda huduma maalumu na kujitofautisha zaidi. Kwa mawasiliano zaidi:www.tib.co.tz
TIB Rasilimali Ltd ni taasisi ya tatu katika muundo huu wa TIB Group inayojihusisha na masuala ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kama vile ununuaji na uuzaji wa hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la hisa Dar es salaam (DSE). Pia kutoa ushauri wa kifedha na kuwezesha utafutaji wa mitaji.
TIB Rasilimali ndio wakala pekee wa soko la hisa la Dar Es salaam inayomilikiwa na serikali. Imesajiliwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana(CMSA),pia inajihusisha na masuala ya usimamizi wa fedha (fund management) chini ya usajili wa Mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya jamii (SSRA).Kwa mawasiliano zaidi:[email protected]