×

VIDEO: Rais Magufuli Azindua Mradi wa Maji Nyamazugo Sengerema, Atoa Kauli Nzito

 

Rais Dkt. John Magufuli amezindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema leo ambapo mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh23 bilioni utawanufaisha zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo zaidi ya 13,000 na utahudumia kata 11.

 

Kata hizo ni Sima, Nyatukala, Ibisabageni, Mwabaruhi, Nyampulukano, Misheni, Tabaruka, Nyampande, Nyamazugu, Nyamazeze na Ibondo.

 

Mhandisi wa Maji Wilaya ya Sengerema, Nikas Ligombi alisema mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Afrika umekamilika kwa asilima 100 na utakapozinduliwa rasmi tatizo la maji katika mji wa Sengerema litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

 

“Lita za ujazo 150,000 zitakuwa zinasukumwa kila siku kutoka kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye matanki ya kusambaza mitaani,” alisema Ligombi.

 

 

Yaliyojili kwenye uzinduzi huo;

Leave a Comment