
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mganda, Emannuel Okwi, anatarajia kuwasili nchini Julai 17, mwaka huu baada ya kumalizika mechi ya Chan ambapo Uganda itacheza na Sudan Kusini.
Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba ambapo kwa sasa yupo nchini kwao akisubiri kuitumikia timu yake ya taifa kabla ya kujiunga na na wenzake mara baada ya kumaliza mechi ya Chan ambayo inachezwa Julai 15, mwaka huu.
“Wachezaji wote waliokuwa timu ya taifa watajiunga baada ya tarehe hiyo, ndipo wachezaji wote watakapoungana kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu.
“Wachezaji wote wa kimataifa tayari wameshatumiwa tiketi, wale ambao hawapo katika timu za taifa watatua nchini kuanzia Alhamisi hadi mwishoni mwa wiki hii,” alisema Abass.
wenzake Msimbazi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mratibu wa Simba, Abass Ally, ameeleza kuwa, mshambuliaji huyo atajiunga.
Stori na Khadija Mngwai