
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema kuondoka kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu ndani ya kikosi chao hakutakuwa na pengo na anamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya Yanga.
Ajibu amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga baada ya kumaliza mkataba wake wa kuichezea Simba hivi karibuni.
Jumatano wiki hii, Yanga ilimtambulisha Ajibu kuwa mchezaji wake na kumpa jezi namba 10 baada ya kukamilisha usajili wake wa Sh milioni 50.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkude amesema kuwa, Ajibu ni mchezaji mzuri lakini kuondoka kwake Simba hakumaanishi kutakuwa na pengo lake kwani kuna wachezaji wengine wa kuziba nafasi yake.
“Siwezi kumbeza Ajibu kwenda Yanga, kwani hadi viongozi wa timu hiyo wameamua kumchukua kuna kitu wamekiona ndani yake, ni mchezaji mzuri ana uwezo mzuri na ndiyo maana amesajiliwa.
“Kuondoka kwake hakutakuwa na pengo katika kikosi chetu kwani naamini wachezaji waliosajiliwa na watakaosajiliwa wataleta ushindani na kuifanya Simba ifanye vyema kwenye ligi na katika michuano ya kimataifa,” alisema Mkude.
Simba msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara na Kombe.