
WASOMAJI wa Vitabu vya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo wameombwa kufika katika banda la AIC lililopo, Barabara ya Karume kwenye Maonesho ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa utawala wa taasisi ya ubunifu wa biashara ya kilimo (Agribusiness Innovation Center), Sandra Nassoro alisema kuwa wasomaji waendelee kufika kwenye banda hilo kwani wataweza kununua vitabu hivyo vya Shigongo ambaye ni mhamasishaji mahiri hapa nchini wa ujasiriamali na watapewa pia maelekezo namna vinavyopatikana.
Mbali na vitabu hivyo, pia banda hilo ni la taasisi ya ubunifu wa biashara ya kilimo ambayo inajuhusisha na kukuza biashara za wajasiriamali na wasindikaji wenye mlengo wa kukua kibiashara.
Akielezea kuhusu taasisi hiyo inavyohusika alisema kuwa inawasaidia wajasiriamali kuwatafutia mitaji ya biashara na kutoa udhamini wa hadi asilimia 80 wa kiasi cha mkopo kwa kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.
Tunawaunganisha na wauzaji wa mashine za usindikaji na kuwapa maarifa ya udhibiti wa fedha za biashara pamoja na kuwaunganisha na mitandao ya biashara.
NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS
===