





Jumamosi iliyopita, wafanyakazi wa Global Publishers walipata fursa ya kwenda kujiachia kwenye ufukwe wa Hawaii ulioko Bahari ya Hindi eneo la Boko ambako walijirusha kwa kuogelea, kula chakula cha mchana, wakacheza mpira wa miguu, wakacheza muziki, wakakimbia na kufanya kila tukio la furaha.
Madhumuni ya kujiachia huko ni kuondoa ‘stress’ za kazi na kujenga afya mpya na kupata mawazo mapya kwa kujiburudisha na mambo mbalimbali ambapo baadaye makulaji na mwanyaji yaliendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Shavila Hoteli iliyoko Tegeta. Hapo walipata tena vyakula na vinywaji mbalimbali ambapo muziki uliendeleza shamra zote hizo hadi kunako saa tano za usiku.