×

Wafanyakazi wa Global Wakijiachia Ufukwe wa Bahari ya Hindi

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika ufukwe wa Hawaii Beach iliyoko katika Bahari ya Hindi eneo la Boko, Jumamosi.
Said Ally (kulia), Abdallah Kipunde (katikati) na Ayoub Laurent wakila bata ufukweni hapo.
Mayasa Mariwata (kushoto) na Lucy Mgina aka ‘Minaj’ wakijirusha.
Sweetbert Lukonge akifanya yake ndani ya bahari.
Wafanyakazi wakiendelea kujinafasi.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Amran Kaima (aliyekaa chini) akiwa na Musa Mateja (katikati) na Elius Kambili wakifurahia mandhari ya ufukwe huo.

Jumamosi iliyopita, wafanyakazi wa Global Publishers walipata fursa ya kwenda kujiachia kwenye ufukwe wa Hawaii ulioko Bahari ya Hindi eneo la Boko  ambako walijirusha kwa kuogelea, kula chakula cha mchana, wakacheza mpira wa miguu, wakacheza muziki, wakakimbia na kufanya kila tukio la furaha.

Madhumuni ya kujiachia huko ni kuondoa ‘stress’ za kazi na kujenga afya mpya na kupata mawazo mapya kwa kujiburudisha na mambo mbalimbali ambapo baadaye makulaji na mwanyaji yaliendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Shavila Hoteli iliyoko Tegeta.  Hapo walipata tena vyakula na vinywaji mbalimbali ambapo muziki uliendeleza shamra zote hizo hadi kunako saa tano za usiku.

Leave a Comment