×

Dua kwa Wasanii Nazo ni Kiki?

Dida akifanyiwa kisomo.

 

KUMEKUWA na tabia inayozidi kuota mizizi kwa baadhi ya wasanii, watangazaji na hata wafanyakazi wa nyanja mbalimbali kuamini katika nguvu nyingine nje ya uwezo wa kawaida wa kazi zao, kama vile kushiriki vitendo vya kishirikina, kufanya ibada kwa mujibu wa madhehebu ya dini zao na vitu vingine vya namna hiyo.

Hali hii inafanyika pale wanapohisi kuwepo kwa ushindani mkubwa katika kazi zao kama ilivyo sasa katika muziki wa kizazi kipya na filamu. Dhana ya watu kukimbilia kwa waganga wa kienyeji, wanajimu na kwenye maombi haijaanza leo.

Kumekuwa na maoni tofauti juu ya uwezo wa nguvu za kishirikina katika kutimiza matakwa ya mhitaji, kama ambavyo wamegawanyika katika kuamini maombi yanayofanywa na wahubiri, wachungaji, mashehe na watu wengine wa aina hiyo.

Mara nyingi katika shughuli za imani za kishirikina, wengi hufanya siri, kwani huamini zina matokeo hasi, hasa kwa kuwa kuna kuharibiana nyota, kuvuta nuru kwa nguvu za giza na vitu vingine kama hivyo.

 

Wema alivyofanyiwa kisomo.

 

 

Lakini kuna hawa ambao wamekuwa wakitafuta vitu hivyo kwa kufanya maombi pia kwa mashehe, wachungaji, makanisani, misikitini na hata katika ibada maalum zinazofanyika majumbani.

Katika maombi kila mmoja ana jinsi ya imani yake katika kupata wokovu anaoutarajia, maana hata kwenye nyumba za ibada, si wote ambao huliita jina la Mungu humaanisha hivyo katika matendo yao.

Kuna wasanii wengi wenye kashfa ya kufanya ushirikina ili waendelee kufanya vizuri katika muziki wao. Baadhi yao wamekutwa ‘red handed’ kwa waganga wa kienyeji wakifanya vitu vyao, wengi pia wamekutwa wakifanyiwa visomo ili kuondoa kile wanachosema, mikosi na mabalaa.

Wema Sepetu

 

Baadhi ya watu mashuhuri ambao wamewahi kufanyiwa dua maalum ili kuondoa kile wanachoamini ni mikosi, ni pamoja na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, ambaye alifanyiwa hivyo muda mchache tu baada ya kuachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, alikoshikiliwa kwa siku kadhaa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya.

Wema alifanyiwa hivyo kwa dhana kwamba kilichomtokea ni mikosi na mabalaa hivyo ni vyema vitabu vitakatifu vikasomwa ili kusafisha hali ya hewa.

Mwingine aliyejitokeza hadharani na kufanyiwa maombi kwa kile alichodai kuondoa mikosi na mabalaa baada ya kunusurika kifo ajalini, ni mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha Times FM cha jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambaye wiki tatu zilizopita alichomewa ubani na kuangushiwa dua maalum mjini Morogoro, akifanyiwa hivyo na Shehe wa Msikiti Mkuu wa mkoa huo, Alhaj Masenga.

Mmoja wa mashehe wanaofanya ibada na visomo, Salum Mkumba, wa Chanika jijini Dar analizungumzia jambo hilo alipoulizwa kama inafanya kazi au ni kiki tu ya wasanii.

“Mungu anasikiliza maombi ya kila mja wake, inategemea na mhitaji jinsi alivyo na imani kwa Mola wake. Kama wanakwenda kufanyiwa kisomo lakini wakiwa na vitu vyao kichwani, ni wazi kuwa Mwenyezi Mungu hatapokea maombi yao.

 

Stori: Risasi Vibes

Leave a Comment