
MAELFU ya raia wa wanaoishi katika mkoa wa Idlib nchini Syria wamekimbia makazi yao kutokana na vita vinavyoendelea katika maeneo hayo.
Vikosi vya serikali nchini Syria vimeikamata miji na vijiji kadhaa kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa wanamgambo baada ya makabiliano yanayosababisha raia kuyakimbia makazi yao.

Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan, ameonya kuhusu wimbi jipya la wahamiaji katika nchi yake, kwani zaidi ya raia 80,000 wamekimbilia katika mpaka wa Uturuki.