×

Vijana Waelimishwa Mbinu za Kuendeleza Biashara

Mwongozaji wa semina hiyo, Jumanne Mtambalike, akifanya mahojiano na mshiriki wa semina hiyo.

 

MHAMASISHAJI mashuhuri wa kimataifa na Mwenyekiti Mtendaji wa Mawasiliano ya  Simu ya Econet  na Vyombo vya Habari na Teknolojia Dk. Strive Masiyiwa,  jana usiku alielezea mbinu mbalimbali zinazoweza kuwafanya vijana kuondokana na umaskini.

 

 

Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo.

 

Aliyasema hayo katika semina  iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, ambapo jumla ya washiriki 500 walihudhuria kujifunza mambo mbalimbali ya kiuchumi na kimaendeleo, wengi wao wakiwa vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali nchini.

 

Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo.

 

Aidha,  Dk. Masiyiwa alifafanua namna vijana wanavyoweza kutoka  hatua moja hadi nyingine ya kimaendeleo kupitia fursa wanazozifanya, na alielezea kirefu elimu ya ushauri wa kimawazo katika jamii ambayo ni muhimu kwa kuwajenga wajasiriamali barani Afrika.

 

Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo.

 

Baadhi ya vijana waliohudhuria wa semina hiyo.

 

Mkurugenzi wa kituo cha Televisheni cha TV-E, waliokuwa wadhamini wakuu wa semina hiyo, Joseph Sayi, akizungumza baada ya kumalizika kwa semina hiyo.

 

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment