
Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba kusimamisha kuwapa uraia raia wa Burundi kuanzia sasa na kuwaomba warejee kwao kama alivyowataka Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kwa vile nchini humo sasa amani imerejea.
Hayo ameyasema leo, Alhamisi Julai 20 wakati akizungumza katika Uwanja wa Mpira wa Lemela, Ngara alipokwenda kwa ziara yake mkoani Kagera, akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
“Rais amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka kwenu?
“Naomba Warundi mrudi nyumbani, mkashirikiane na wenzenu kuijenga Burundi. Nchi ina amani sasa, wala asitokee mtu akawadanganya kwamba kuna machafuko. Hatuwafukuzi lakini tunawaomba muende kwa amani, nyinyi ni ndugu zetu,” alisema Magufuli.
Awali, Rais Nkurunziza amezungumza na wananchi hao na kuwataka raia wa Burundi warudi nchini mwao kwani kwa sasa amani imerejea.
Kadhalika, Waziri Nchemba amesema katika kipindi cha 2016/17, Tanzania imewapa uraia wakimbizi wa Burundi 1,060 akaongeza kwamba kati ya wakimbizi 247,000 waliopo nchini, 5,000 wameomba kurudi kwao.
=============
YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO HUO
NGARA: Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewasili uwanja wa mpira wa Lemela, Ngara, Kagera na kupokewa na Rais Magufuli asubuhi hii.
Rais Magufuli amesema mazungumzo yake na Rais Nkurunziza yamehusu ushirikiano wa biashara na ujenzi wa reli kutoka Dar, Rwanda na Burundi.
NGARA: Rais @pnkurunziza amewataka wakimbizi wa Burundi walioko Tanzania warudi kwao wakajenge nchi yao kwani kwa sasa hakuna machafuko.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
NGARA: Rais Magufuli amemuagiza waziri wa mambo ya ndani kusitisha mara moja kutoa uraia wa Tanzania kwa wakimbizi wa Burundi na badala yake warudi kwao.
Rais @MagufuliJP amesema atanunua pampu kubwa ya maji yenye gharama ya Tsh. Mil 13 kwa wakazi wa Ngara ili kutatua tatizo la maji eneo hilo pic.twitter.com/GKCL3ZfpZb
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
#JPMNgara: Mkurugenzi unashindwa kupeleka maji kwa wananchi 20,000 unapeleka kwa wanajeshi 200. (1/1)
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
#JPMNgara: Nataka hizo mil. 200 zitekeleze mradi wa maji kwa wananchi, hao wanajeshi niachie mimi na CDF.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
#JPMNgara: Nafahamu kwa sasa tatizo la umeme limepungua, mpango wa REA awamu ya pili nitaleta umeme hapa ili kulimaliza kabisa tatizo hili.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
NGARA:Mkazi wa Kanazi,Anthony amueleza @MagufuliJP kuwa wananchi wananyimwa ardhi ya kulima na mamlaka husika, JPM amuagiza RC kushughulikia pic.twitter.com/cq3NkVXGJG
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 20, 2017
FUATILIA MKUTANO HUO HAPA