×

Irving Aomba Kumkimbia James

Mchezaji wa Cleveland Cavaliers, Kyrie Andrew Irving.

PAMOJA na kwamba kila usajili kwenye Ligi Kuu ya Kikapu Marekani (NBA), umekuwa ukishangaza, lakini kama dili la Kyrie Irving la kuondoka kwenye timu ya Cleveland Cavaliers likitiki, litashangaza zaidi.

Staa huyo ambaye alionyesha kiwango cha hali ya juu msimu uliopita, wiki iliyopita ilitangazwa kuwa ameieleza klabu yake kuwa imuuze. Hata hivyo, taarifa ambazo siyo rasmi zinasema kuwa staa huyo ameomba kuondoka kwa kuwa hataki tena kucheza timu moja na staa wa NBA, LeBron James.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, msimu uliopita alishika nafasi ya pili nyuma ya James kwa kufunga wastani wa pointi 25.4.

…Akiwa Uwanjani akifanya yake

Pamoja na mafanikio ambayo ameyapata kwenye timu hiyo, bado Irving ameona jambo la msingi kwake ni kuondoka pamoja na kwamba James amefanya kazi kubwa sana tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2014.

 

Tangu James ajiunge na timu hiyo, imefanikiwa kufika fainali mara tatu, huku ikitwaa ubingwa wa NBA mwaka 2016, baada ya Cavs kutoka nyuma kwa michezo 3-1.

Wakala wa Irving, Jeff Wechsler, alinukuliwa Ijumaa iliyopita na Mtandao wa NBA akisema : “Ninachoweza kusema ni kwamba tulikuwa na mkutano wiki kadhaa nyuma, tulikaa na kujadili kuhusu mustakabali wa Kyrie, matokeo ya mkutano huo tutayaweka wazi hivi karibuni.

Leave a Comment