×

Wafanyakazi Tanesco Waahidi Kuchapa Kazi Kufa na Kupona

Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano, Hassan Athuman akizungumza na wanahabari.

 

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa umoja wao kupitia Chama Cha Wafanyakazi (TUICO) wametoa pongezi za dhati kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa mchango wake mkubwa wa katika kuendeleza sekta ndogo ya umeme kwa kulipa nguvu shirika hilo katika kutekeleza majukumu yake na pia kuahidi kufanya kazi kwa nguvu zao zote wakati wowote, mahali popote.

 

Akizungumza katika hafla fupi, Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano, Hassan Athuman amesema kuwa Tangu kuingia madarakani serikali ya awamu ya tano imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shirika hilo linajiendesha kwa ufanisi ili kufikia azma ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda.

 

Mkutano ukiendelea.

 

“Rais Magufuli amewezesha TANESCO kukusanya mapato yake kwa kasi na nguvu zaidi, kazi ambayo ilikuwa ikikubwa na changamoto nyingi hususan katika ulipaji wa madeni ya umeme ya maeneo nyeti Kama taasisi mbalimbali za serikali, pia katika ukusanyaji wa deni la umeme la Zanzibar.

 

“Kutokana na Kampeni ya “KA-TA” iliyoasisiwa na Rais Magufuli imewezesha kukusanya deni la umeme kwa kiasi kikubwa jambo ambalo hapo awali haikuwa rahisi,” alisema Athuman.

 

Ameeleza kuwa kabla ya agizo la mheshimiwa rais uwezo wa ukusanyaji mapato ya shirika ulikuwa ukifikia asilimia 90, lakini baada ya tamko la rais wameweza kukusanya asilimia 104 ya deni lote la umeme kwa wadaiwa sugu.

 

TAZAMA VIDEO YA MKUTANO HUO

Leave a Comment