×

Wenye Smart Phone Wapewa ‘Maujanja’ Kusoma Magazeti Mtandaoni

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Samuel Eric (wa kwanza kushoto aliyechuchumaa) akiwaelekeza wasomaji wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers Ltd, wa maeneo ya Mburahati namna ya kuyasoma kwa njia ya kidijitali yaani kupitia Global App au Website ya www.globalapp.co.tz.

WAKATI Kampuni ya Global Publishers Ltd ikizidi kwenda kasi katika ulimwengu wa kidijitali  mtandaoni,  leo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo wameendelea na zoezi lao la kutoa elimu juu ya namna wasomaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani wanavyoyapata kwa njia ya kidijitali.

Kazi kubwa ya kampuni hiyo ni kuhakikisha inawajali wasomaji wake katika mapinduzi ya ulimwengu wa kidijitali na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).

Maofisa hao wameingia tena mtaani kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kuhusiana na kuyasoma magazeti hayo kwa njia ya mtandao. Katika kuzunguka kwao wameweza kutembelea maeneo ya Mabibo, Kigogo, Mburahati na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam kuendelea kuhamasisha wasomaji wa Magazeti Pendwa kuendelea kujipatia uhondo wa habari za burudani kupitia mtandaoni.

…Akimwelekeza msomaji  Soko la Kigogo Sambusa, Aly Chaurembo, namna ya kuyasoma  kidijitali.

Akizungumza na wasomaji wa maeneo hayo,  Eric amesema kuwa Kampuni ya Global katika kuhakikisha inawajali wasomaji wake na wanaendana na kasi ya ulimwengu wa teknolojia, wameamua kuwawekea magazeti hayo kwa mfumo huo  ili kuwarahisishia na kuokoa muda wao  ambao walikuwa wakiupoteza kwa kwenda katika meza za wauzaji na hata kukosa kabisa muda wa kuyafatilia.

 

“Naomba wasomaji wetu mtuelewe; tumeamua kuwarahisishia muyapate Magazeti yetu Pendwa kupitia njia ya mtandao.  Hii yote ni kutokana na dunia inavyokimbia kasi katika ulimwengu wa teknolojia ambapo  tutaendelea kuwajali kwa kuwapatia habari motomoto kupitia mtandao tena kwa bei ya Tsh 300/= kuanzia mwezi ujao wakati kwa mwezi huu yakipatikana bure mtandaoni.

Mkuu wa kitengo cha masoko, Anthony Adam (kushoto) akiwaelekeza wasomaji namna ya kuyapata magazeti kupitia mfumo wa kidijitali.

Mmoja wa wasomaji wa Magazeti Pendwa aliyejitambulisha kwa jina la Ally Chaurembo mkazi wa Kigogo-Sambusa ameipongeza Kampuni ya Global Group kwa kuendana na kasi ya teknolojia akisema kuwa uwepo wa magazeti hayo mtandaoni utamsaidia kuokoa muda  aliokuwa akiutumia ambapo badala yake atatumia simu yake ya mkononi kufanya malipo na kusoma.

 

“Global mmetufanyia jambo jema; ukiangalia mimi nafanya biashara zangu hapa soko la Kigogo-Sambusa ambapo hakuna hata meza ya magazeti.  Ilikuwa inaniwia ngumu kuyafuatilia umbali mrefu lakini kwa sasa natumia simu yangu kusoma na hata kama nimebanwa na kazi,  nikifika nyumbani najisomea kupitia simu.  Asanteni sana kwa kuturahisishia,” alisema Chaurembo.

…Akimwelekeza msomaji  jinsi ya  kuyapata magazeti  kupitia mfumo wa kidijitali ambako hivi sasa yanapatikana.

Kwa msomaji, ili kuyasoma magazeti hayo ni ku-download application yako ya Global Publishers ili usome hadithi uzipendazo na habari za magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani, BURE kwa mwezi mzima  hivi sasa sasa!

 

Baada ya OFA hii, utayasoma kwa bei rahisi ya shilingi 300 tu kwa nakala popote ulipo, ndani na nje ya Tanzania, kupitia Global App au website ya www.globalapp.co.tz #GlobalApp #GlobalPublishers #Uwazi #Risasi #Amani #IjumaaWikienda
Pakua App ya Global kwenye Google Playstore, App Store.
⚫ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫ iOS:https://apple.co/3msGaf8

Wasomaji wakipata maelezo ya kuyasoma magazeti kidijitali.

Leave a Comment