The House of Favourite Newspapers

KISA: SEDUCE ME, CHRISTINA SHUSHO AMUITA KIBA KANISANI

0

mkali wa Bongo Fleva

IKIWA ni siku mbili tu tangu, mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’, aachie kibao chake cha Seduce Me, ngoma hiyo imeendelea kukuna mioyo ya mashabiki wake, akiwemo muimbaji wa Injili nchini Christina Shusho, ambaye ameweka wazi mapenzi yake juu ya ngoma hiyo kwa kuposti katika ukurasa wake wa Instagram.

mkali wa Bongo Fleva

“Leo unaweza kukuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha Seduce Me, Eeh jamani Kiba we noma, wimbo ni mzuri sana kitaaluma kama anavyopenda kusema bosi Ruge.

“Hauna picha za aibu , naweza kuuangalia nikiwa na familia, labda sijui maana ya Seduce Me. Timu Kigoma
Wamanyema oyeeeee.

 

“Cha mwisho Ali Kiba basi siku nyingine tutembelee kanisani ukiwa mfalme huchagui dini wote wako” ameandika Christina Shusho.

mkali wa Bongo Fleva

Licha ya kuwa na siku mbili tu tangu utoke, wimbo huo wa Kiba, umevunja rekodi ya kutazamwa na zaidi ya watu milioni moja ndani ya masaa 38

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Leave A Reply