The House of Favourite Newspapers

Shuhudia LIVE Mti wa Maajabu Unaotoa ‘Damu’, Upo Hapa Hapa Bongo!

1

KAMA ada yetu, jukumu kubwa la GLOBAL TV Online ni kukusogezea matukio yote muhimu ambayo wewe mdau wetu una kiu ya kuyafahamu muda wowote na wakati wowote.

Kwa mara nyingine tena, Global TV imefunga safari mpaka Mkoani Mbeya, Wilaya ya Rungwe, Kata ya Kisiba kijiji cha Lugombo ambapo kuna Himaya ya Chief Mwambuga. Eneo hilo kuna mti wa kustaajabisha.

MAAJABU YA MTI KATEMBO, UPANDE UTOMVU MWEUPE, UPANDE DAMU!

Mti huu ni aina ya Mvule maarufu kwa jina la Mti wa Katembo, unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 au zaidi. Ukubwa wake wa duara unahitaji watu kuanzia wanane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa.

Inaelezwa kuwa Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja ambalo, hata ukifika leo panaonekana, inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani.

GLOBAL TV ONLINE imefika eneo la tukio na kuongea na viongozi wa kijiji na kushuhudia huo mti ukitoa utomvu wa damu.

SHUHUDIA MTI HUO HAPA

 

 

Usipitwe na Matukio, Download na Install ==> Global Publishers App

1 Comment
  1. […] nilipogeuka nyuma, nilimuona mtu wa ajabu akizidi kunikaribia. Nikaongeza mbio ili kujiweka salama. Hata hivyo, kwa sababu ya kukimbia kupita […]

Leave A Reply