×

SHAKA SSALI AZULU GLOBAL PUBLISHERS

Mtangazaji maarufu kutoka Kituo cha Sauti ya Amerika (VoA), Shaka Ssali akiwa ndani ya Global TV Online kabla ya kuanza kufanya mahojiano.
Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric James Shigongo  akimtambulisha Shaka Ssali kwa wafanyakazi wa Global Publishers.
Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kulia) akiwa na Shaka Ssali.
Mahojiano yakiendelea, kulia ni mtangazaji wa Global TV Online, Catherine Kahabi.
Shaka Ssali akiweka saini kitabu cha wageni. 

MTANGAZAJI wa kimataifa kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VoA) ambaye ni mhariri na mtangazaji wa Kipindi cha Straight Africa Talk, Shaka Ssali mapema leo ametembelea Ofisi za Global Publishers na kufanya mahojiano maalum.

 

Katika mahojiano na chaneli namba moja ya mtandaoni  ya Global TV Online, Shaka alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kujitoa kwa hali na mali, katika kuhakikisha wanadumisha upendo na amani huku akitumia nafasi hiyo pia kuwataka baadhi ya viongozi wa Afrika kuhakikisha wanatimiza majukumu ya kukuza na kuendeleza demokrasia na kuhudumia wananchi kwa kiwango bora.

 

Pia, Shaka Ssali ambaye atakuwa ni miongoni mwa wageni na wazungumzaji wa Tamasha la Meza ya Uzalendo, linalotarajiwa kurindima Septemba 2, 2017 kwenye Ukumbi wa Nkurumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kudumisha uzalendo kwa nchi zao na zaidi sana kuhakikisha wanakimbiza na kutimiza ndoto zao maishani, ikiwa ni pamoja na kujitolea kwa moyo wote kujenga nchi zao.

 

“Nimefurahi sana kutembelea Global Publishers, lakini pia nimeona namna ambavyo mnaonekana kuwa na juhudi za kupambana na maisha, tupendeni sana kudumisha uzalendo wetu, viongozi wa  Afrika nao waendelee kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa wananchi, pia vijana ni muhimu kupigania ndoto za maisha yetu kwa kufanya yaliyo mema, kujielimisha vya kutosha juu ya ndoto na malengo yenu, mfano mimi nasoma sana vitabu, na majarida kuhusu kazi yangu, nawapenda sana na Mungu awabariki,” alisema Shaka Ssali.

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave a Comment