×

Sokabet Kuzinduliwa Leo, Mastaa Kibao Kuhudhuria

Muonekano wa tovuti ya Sokabet

KAMPUNI ya Mchezo wa Kubahatisha ya Sokabet, leo Jumatatu inatarajiwa kuzinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam katika hafla fupi itakayofanyika kwenye Hoteli ya Protea.

Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda amesema kuwa katika hafla hiyo pia kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Wabantu Organization.

“Kwa mara ya kwanza kabisa leo Jumatatu Septemba 4, 2017 tunafanya uzinduzi wa kampuni yetu ya Sokabet hapa nchini ambayo inajishughulisha na mchezo wa kutabiri matokeo na uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Protea.

“Tumejipanga vizuri na tunatarajia katika uzinduzi huo tutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Wabantu Organization kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwaomba Watanzania wote kuipokea Sokabet ili waweze kubadili maisha yao,” alisema Ruhinda.

Katika hatua nyingine, kiongozi wa kikundi cha Wabantu Organization, Abdallah Angaly amesema wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kutoa burudani mbalimbali katika hafla hiyo ili kuhakikisha wanazikonga nyoyo za watu wote watakaohudhuria hafla hiyo.

“Sanaa tutakazozionyesha katika hafla hiyo ni ngoma za asili, sarakasi, mchezo wa kucheza na nyoka pamoja na michezo mingine mingi,” alisema Abdallah.

Aidha, katika hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na wachezaji maarufu wa zamani pamoja na mastaa wengine kadhaa wa fani tofauti.

 

Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.

 

STORI: JOHN JOSEPH | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment