
BAADA ya kuanza kimyakimya kupiga mzigo na kuwawezesha Watanzania wengi kuneemeka kutokana na kupatia katika michezo ya kubashiri matokeo, hatimaye Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo ya Sokabet ilizinduliwa juzi Jumatatu na kumwaga shilingi milioni 150 kwa kuidhamini timu ya Majimaji.

Kampuni ya Sokabet ambayo ina wiki chache tangu ilipoanza kupiga mzigo, ilifanya hafla ya uzinduzi wake katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanamichezo mbalimbali wakiwemo wachezaji wa zamani na wa sasa katika medani ya soka, waigizaji na wasanii wengine wengi.

Katika hafla hiyo, uongozi wa Majimaji ukiongozwa na mwenyekiti wake, Steven Ngonyani ulionyesha furaha kwa kupata dili hilo la mwaka mmoja na kuamini litawasaidia kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Tanzania msimu huu ambapo imeshacheza mchezo mmoja na kupoteza mbele ya Mbeya City.

Akizungumzia uzinduzi huo na dili hilo la mkataba, Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda alisema: “Tunayo furaha kuona leo (juzi Jumatatu) tunazindua rasmi Sokabet ambayo itawapa fursa wadau wa kubeti kujishindia mamilioni kwa dau dogo tu watakaloweka kwenye kubashiri kwao michezo mbalimbali ikiwemo soka na ngumi.
“Lakini pia tunayo furaha zaidi kuingia mkataba na Majimaji ambapo kupitia timu hii inayoshiriki Ligi Kuu Bara, Sokabet itatangazwa kila kona na kujulikana zaidi nchi nzima.

“Lengo letu ni kusaidia jamii kwa kuwekeza katika taasisi mbalimbali kadiri tutakavyokuwa tukiingiza, udhamini huu wa Majimaji ni mwanzo wa safari yetu ndefu.”
Upande wa Ngonyani alisema: “Tunashukuru udhamini huu wa Sokabet kwani utatuongezea kitu kwenye timu yetu hususan katika kujiendesha msimu mzima huu wa ligi ambao una mambo mengi, lakini pia tutaitangaza popote tuendapo.”
Baadhi ya wachezaji wa zamani waliohudhuria uzinduzi huo ni Edibily Lunyamila, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, Bakari Malima, Kenny Mkapa, Ally Mayay, Aaron Nyanda, Boniface Pawasa, Manyika Peter na Dua Said.

Wachezaji hao walipongeza ujio wa Sokabet na kusema utaongeza chachu kwa Majimaji na kuonyesha ushindani katika Ligi Kuu Bara.
Mbali na wanasoka hao pia msanii wa vichekesho Haji Salum maarufu kwa jina la Mboto pia alikuwepo kwenye hafla hiyo.
Franco aliongeza kuwa kampuni hiyo ya Kitanzania inaanza ikiwa na mikakati mingi ya kusaidia jamii kwa kile ambacho kitakuwa kikipatikana kutokana na kubashiri, ambapo washiriki wanaweza kujiunga kwa kuingia katika tovuti ya www.sokabet.co.tz.
MWANDISHI WETU, Dar es Salaam
Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.
SHUHUDIA UZINDUZI WA SOKABET