×

G Nako: Tungelegea Saida Angetuficha

Saida Karoli.

RAPA anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, George Sixtus Mdemu ‘G Nako’ amesema kuwa, Saida Karoli ni mwanamama mwenye kipaji cha hali ya juu mno na kama yeye pamoja na Belle 9 wangelegea basi angewaficha kwenye ngoma yake mpya ya Kichaka.

George Sixtus Mdemu ‘G Nako’.

Akichonga na Showbiz, G Nako a.k.a Warawara alisema: Tulikutana na Saida studio tu kila mmoja akiwa na project yake, sasa kuna ngoma ambayo nilikuwa nimeshairekodi kidogo, Saida akaisikiliza na kuipenda akaamua kuichukua na kuingiza sauti, kisha Belle 9 naye akaja kufanya vesi yake.

BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA

Leave a Comment