×

Rashford Akianza Tu, Anatupia

Mshambuliaji chipukizi Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 19.

MANCHESTER United imeanza msimu vizuri, kume­kuwa na matumaini makubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao itafanya vizuri kutokana na kuoneka­na kama imekamilika katika idara nyingi.

Ushindani wa namba ni mkubwa kikosini hapo chi­ni ya Kocha Jose Mourinho, pamoja na hivyo, chipukizi Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 19 ameende­lea kuthibitisha kuwa anao uwezo wa kushindania namba katika kikosi cha kwanza.

Rashford amekuwa na mwen­delezo mzuri wa kile anachoki­fanya kutokana na kasi yake ya ufungaji, kuwasumbua wapinzani na jinsi ambavyo ameweza kuwa tish­io hata kwa walinzi wakongwe.

Usiku wa Jumanne ya wiki hii aliweka rekodi ya kipeke ya kufunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye michua­no ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya FC Basel ambapo United ilishinda kwa mabao 3-0.

Bao moja alilofunga akitokea benchi katika mchezo huo limemfanya kuwa amefunga mabao katika mechi saba za kwanza za michuano ambayo ame­kuwa akianza. Yaani katika kila mechi ya kwanza ya michuano husika amekuwa akifunga.

Tujikumbushe jinsi ambavyo Rashford amekuwa hatari katika michuano saba tofauti aliyopewa nafasi tangu mwaka 2016 ambapo hii inajumuisha klabu na timu ya taifa lake ya England.

Rekodi yake hiyo inaonyesha amefunga katika kila mechi yake ya kwanza ya mi­chuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Eu­ropa League, Premier League, League Cup, England timu ya wakubwa na Eng­land U21:

EUROPA LEAGUE

Man United v Midtjylland

Februari 25, 2016

Katika hii mechi h a k u w e m o k w e n y e

ratiba ya kucheza lakini alilazimika kupangwa na Kocha Louis van Gaal baa­da ya kuumia kwa Antony Martial wakati wa kupasha misuli. United ilipata ushindi wa mabao 5-1 na kufuzu katika Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Alifunga mabao mawili na kuwafanya mashabiki wengi wa United kujiuliza juu ya mfungaji huyo kwa kuwa kocha alilaz­imika kuwatumia chipukizi wengi katika mchezo huo uliopigwa Old Trafford kuto­kana na kuwa majeruhi.

PREMIER LEAGUE

Man United v Arsenal

Februari 28, 2016

Siku chache baadaye United ilikutana na Arsenal ambayo ilikuwa katika ubora mzuri huku wenyeji wakiwa na chipukizi wengi, ilionekana ni suala la Arsenal itashin­da ngapi na siyo timu gani itashinda, lakini Rashford alibadili fikra za mamilioni ya mashabiki wa soka kwa kufunga mabao mawili na kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Old Trafford.

TIMU YA TAIFA

England v Australia

Mei 27, 2016

Alifanikiwa kufunga bao katika dakika ya tatu tu tangu aanze kuichezea timu ya wakubwa ya England, bao lake hilo lilichangia kuiwezesha Eng­land kushinda 2-1 kwenye Uwanja wa Light.

TIMU YA TAIFA

England U21 v Norway U21

Septemba 6, 2016

Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 alimuomba Rashford kutokana na umuhimu wa mchezo huo, ‘dogo’ haku­fanya makosa, kwani alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ na kuchangia England kushinda 6-1 katika mchezo huo wa ku­fuzu Euro 2017.

 

 

Man United v North­ampton

Septemba 21, 2016

United ikiwa ugenini ilishuhudiwa Rash­ford akitokea benchi na kuipa timu yake ushindi katika mechi ya Kombe la Ligi, bao ambalo lilitokana na uzembe wa kipa wa wapinzani zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika, ambapo walishinda mabao 3-1.

LIGI YA MAB­INGWA ULAYA

Man United v FC Basel

Septemba 12, 2017

Akiwa kwenye uwanja wake wa kujidai wa nyumbani, akitokea benchi pia, kija­na alifunga bao katika dakika ya 77 aki­malizia kazi nzuri ya Marouane Fellaini.

Rekodi zinaonyesha katika michuano yote ambayo amecheza, Rashford al­ishindwa kufunga katika mchezo wake wa kwanza wa FA Cup tu, kwingine kote akianza lazima awasalimie kwanza.

Leave a Comment