The House of Favourite Newspapers

Mmiliki wa Nyumba Ya Pili Ya Global Sasa Kujulikana J’5 ijayo

0
Mjengo utakaotolewa na Global Publishers wenye thamani ya mamilioni, uliojengwa Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Sa­laam atapatikana.

BAADA ya miezi sita ya wasomaji wa maga­zeti ya Global Publish­ers, kukata na kutuma kuponi zao kwa ajili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, mwisho wa safari umefika na Jumatano ijayo, itakuwa ndiyo siku ambayo mmiliki wa mjengo huo wenye thamani ya mamilioni, uliojengwa Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Sa­laam atapatikana.

 

Droo kubwa ya bahati nasibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa Septemba 27 mwaka huu, na wasomaji wote ambao bado hawajawasilisha kuponi zao, wanatakiwa kufanya hivyo haraka iwezekanavyo, kwa kuzipeleka kwa mawakala wa magazeti ya Global Publishers waliopo nchi nzima au kwa wakazi wa Dar es Salaam kuz­ipeleka moja kwa moja ofisini kwao, Bamaga Mwenge.

Nyumba hiyo ni ya kisasa yenye vyumba vitatu vya kula­la, kikiwemo kimoja ambacho ni Master Bed Room.

Licha ya vyumba hivyo vi­tatu, ndani ya mjengo huo pia kuna sebule, chumba cha maakuli, jiko na vyoo ndani, kitu ambacho kitamfanya mmiliki wake akiingia ame­ingia. Lakini kitu cha kufura­hisha zaidi kuhusu nyumba hii ni kwamba mmiliki wake, ambaye atakuwa ni yule atakayeibuka mshindi katika droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, hatakuwa na haja ya kuhangaika kuweka umeme, kwani atakuta umeingizwa tayari kwa matumizi.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, ambao ndiyo waendeshaji wa bahati nasibu hiyo, Abdallah Mrisho, alisema jana kuwa ujenzi wote wa ny­umba hiyo umekamilika kwa asilimia mia moja na kwamba mshindi, atajiona wazi jinsi maisha yake yatakavyobadi­lika.

 

“Lengo letu siku zote ni kurejesha faida kidogo tunay­opata kwa jamii tunayofanya nayo kazi, ndiyo maana tume­ingia gharama kubwa kuijen­ga nyumba hii iwe ya kisasa, ili mtu atakayebahatika kuipata, abadili kweli maisha yake na hiyo ndiyo kauli mbiu yetu, ku­badili maisha ya watu.

 

“Ni nyumba ya kisasa kwa vig­ezo vyote, vyumba vitatu vya ku­lala, sebule kubwa, chumba cha chakula, jiko, choo, bafu vyote hivyo vitapatikana ndani ya ny­umba, mmiliki wake atakabidhi­wa hati ya kiwanja na ataukuta umeme umeingia, kazi yake itakuwa ni kuweka luku ili aen­delee na huduma hiyo,” alisema Meneja Mrisho na kuongeza.

 

“Tumekamilisha kila kitu, kilichobakia sasa ni ku­waomba wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Risasi, Championi na Ijumaa kukata kuponi zao za mwishomwisho na kuzituma kwetu haraka iwezekanavyo. Kwa wale wa mikoani, kuponi zao wazipeleke kwa wakala wetu ambao wako kila sehemu nchini.

 

“Kwa wale wa Dar wazilete kuponi zao katika ofisi zetu zi­lizopo Bamaga, Mwenge na wazikabidhi kwa watu maalum wanaozipokea. Huu ni wakati wa kuhakikisha hawakosi naka­la zao kwa vile muda umeshai­sha. Wiki mbili zilizobaki wahak­ikishe hakuna mtu anayeziacha kuponi zake bila kuzileta kwetu, kwa sababu huenda ile utakay­oiacha nyumbani, ndiyo iliy­okuwa ya mshindi.”

 

Nyumba hiyo ya kisasa im­ejengwa Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa na thamani ya mamilioni ya shilingi na itakuwa ni ya pili kutolewa na Global Publishers, kwani katika bahati nasibu ya kwanza iliyo­fanyika mwaka jana, mjengo wa aina hiyo ulitolewa.

 

Aliyeshinda katika bahati na­sibu hiyo ya kwanza alikuwa ni mwanamama mjasiriamali, Nelly Mwangosi mwenyeji wa Iringa ambaye mjengo wake uli­jengwa eneo la Salasala, pia nje ya jiji hili.

 

Bahati Nasibu ya Shinda Ny­umba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali ji­jini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikien­da waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisa­sa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.

LIVE: Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Yaagwa Lugalo

Leave A Reply