×

Familia Ya Jini Kabula Yawashukuru Watanzania!

Jini Kabula.

FAMILIA ya msanii wa Bongo Movie, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ imetoa shukrani za dhati kwa wote walioguswa na kujitolea michango yao ya matibabu ya msanii huyo anayetajwa kuwa na matatizo ya akili na kwamba hadi sasa anaendelea vizuri.

Katika mazungumzo na mwandishi wetu, mmoja wa ndugu wa Kabula, Dynes Jolwa, alisema Watanzania wengi walijitolea kwa michango yao ambapo jumla ya Tsh. 1,070,000/= (milioni moja na elfu sabini) zimekusanywa kupitia mtandao wa simu ya mkononi.

“Kwa niaba ya familia ya Jolwa, napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kuwashukuru Watanzania wote waliojitolea michango yao kuhakikisha matibabu ya ndugu yetu Miriam (Jini Kabula) yanafanikiwa na hata wale ambao hawakutoa pesa taslimu lakini maombi yao yamekuwa msaada mkubwa kwa mgonjwa na kwa sasa tunamshukuru Mungu kwamba anaendelea vizuri, Mungu awazidishie pale palipopungua,” alisema Dynes.

Hata hivyo, Dynes alisema kwa sasa Jini Kabula amehamishiwa mkoani Tanga kwenye Hospitali ya Mission kwa hatua zaidi za kimatibabu na kwamba taarifa za maendeleo yake zitakuwa zinatolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti ya Global Publishers, ambayo ni Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

BRIGHTON MASALU

 

Irene Uwoya: Napenda Mwanaume Mwenye Sura ya Kiume

Leave a Comment