Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kuamkia leo Jumamosi ilipiga bonge la shoo kwenye Ukumbi wa Baa ya T Garden iliyopo Sinza Jijini Dar ambapo nyomi la mashabiki lilihudhuria.
Bendi hiyo inayotamba na ngoma yake mpya ya Mapenzi Sigala Kali utunzi wake, Chaz Baba ‘Kingunge’ mashabiki wamekuwa wakidata sana na kibwagizo cha ngoma hiyo kisemacho msaliti “Msaliti hata weeewe eewe” na uchezaji wa staili ya Maria Roza “Mariaaa eeeh Maria Roooza”
Angalia matukio yalivyokuwa.





Mcharaza besi gitaa, Jojoo Jumanne na muimbaji, Saleh Kupaza wakiwa kazini.
HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL