
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Jumamosi inacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa timu yetu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michuano ya mataifa Afrika Afcon ambayo itafanyika mwaka 2019. Hili litakuwa ni jambo jema kwetu ikiwa kutakuwa na nia ya dhati ya kutaka kulifanikisha jambo hili.
Mchezo wa leo upo katika Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ambao faida yake kubwa ni kuweza kusaidia kupanda katika viwango vya Fifa. Kuna kila sababu ya wachezaji wetu wakalitambua jambo hilo ili kuweza kututoa tulipo. U k i a n galia kwa sasa katika timu yetu tunaweza k u s e m a kuna afadhali ya uwepo wachezaji wanaocheza soka la kulipwa kitu ambacho kilikuwa tatizo kubwa kwa muda mrefu lakini uwepo wao hauwezi kutosha kusaidia kupata matokeo ma- z uri iwapo hakutakuwa na ushirikiano kati yao.

Leo hii katika timu yetu imekuwa ni jambo kubwa kuona tunaita wachezaji wakitokea nje, nahodha Mbwana Samatta, Simon Msuva, Abdallah Hamisi, Farid Mussa, Abdi Banda na wengineo ambao huenda bado hawajaulikana.
Kitu kikubwa ambacho ninachotaka kukisema ni lazima shirikisho la soka liweke mikakati ya kweli katika kuhakikisha timu yetu inaweza kufanya vizuri, kambi bora na uwepo wa wadhamini huenda vikawa havitoshelezi katika kufikia malengo.
Lakini kabla ya kucheza na Malawi, tumeona mchezo wa uliopita tulicheza na Botswana ambao tulifanikiwa kuwafunga, siyo kitu kibaya kwa timu ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki michuano mikubwa.
Stars imekuwa kicheza mechi nyingi katika uwanja wa nyumbani kuliko nje lakini kwa timu ambazo uwezo wake nao hauwezi kuwa kipimo cha uhakika katika kutafuta nafasi ya kushiriki Afcon, lazima TFF itengeneze mpango mkubwa wa mechi kubwa za kirafiki tena za kuchezea ugenini naamini itasaidia kutambua ukubwa wa timu yetu.
Sasa leo tusiwe tunafurahia wachezaji wetu kwa kuweza kupata matokeo ya ushindi kwa mechi ambazo tunacheza hapa lakini timu ikitoka nje inakuwa kinyume chake kitu ambacho kitapelekea tusiweze kupiga hatua.
Mwisho niwatakie kila la kheri katika mchezo huo ambao naamini hautokuwa mwepesi kulingana na timu ambayo tunacheza nao kwa kuwa hata wao wamekubali kucheza na timu yetu wakiamini ni kipimo kizuri kwa ajili ya kuijenga timu yao. Kwa upande mwingine naendelea kusisitiza katika Ligi Daraja la Kwanza bado kuna haja kubwa ya kuwepo wa wadhamini ambao wataweza kuisaidia kuimarisha ushindani wa kweli kwa kuwa msimu ujao ligi hiyo inatarajia kutoa timu sita kwa ajili kuzipeleka kwenye ligi kuu msimu ujao.
TFF bado inapaswa kuliangalia hili mara mbili kwani inakuwa ina vunja moyo hata zile timu za vijana maana itasababisha timu hata vijana wenyewe ambao wengi ndiyo tegemeo la kesho kushindwa kujikita katika mchezo wa soka na matokeo yake wageuke mambo mengine ambayo huenda hayatokuwa bora kwao.
Tunaona wadhamini wengi wakimbilia katika ligi kuu pekee na kuacha kwenye ligi daraja la kwanza kukiwa hakuna mpya hali ambayo imekuwa ikisababisha ugumu mkubwa timu ambazo zinashiriki kushindwa kufikia malengo. Ni wazi sehemu ya uidhamini katika daraja la kwanza ungekuwa basi ingekuwa rahisi kwa timu nyingi kuweza kupata wadhamini ambao wangeweza kusaidia kitu fulani.