The House of Favourite Newspapers

Makundi Ligi Ya Daraja La Tatu Tanga Ni Noma

0

BAADA ya ratiba ya makundi ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Mkoa msimu wa 2017/18, kuwekwa hadharani imeonekana hakuna kundi jepesi na yote kuonekana ya kifo ambapo ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 17, mwaka huu.

 

Ligi hiyo inashirikisha timu 16 kutoka katika wilaya zote mkoani hapa, zikipambana kugombania ubingwa ambao kwa sasa upo mikononi mwa Sahare All Stars.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA), Beatrice Mgaya, alisema makundi yatakuwa manne na katika kila kundi, timu mbili zitakazoshika nafasi za juu, zitaingia hatua ya nane bora, huku timu zitakazoshika nafasi za mwisho katika makundi yao, zitashuka Ligi Daraja la Nne.

 

Bosi huyo wa TRFA aliyataja makundi hayo kuwa Kundi A litakuwa na timu za Muheza United (Muheza), Bomboka FC (Tanga), Korogwe United (Korogwe) na Kwalaguru FC (Handeni), Kundi B lina timu za Jeshi Warriors (Tanga), Kwamndolwa FC (Korogwe), Veteran Middle Age (Tanga) na Beach Boy (Muheza), Kundi C ni Sahare All Stars (Tanga) ambaye ndiye bingwa mtetezi, Majengo United (Tanga), New Star (Handeni) na Halmashauri (Korogwe) huku Kundi D likiwa na timu ya Small Prison (Tanga), Mkanyageni FC (Muheza), Eagle Rangers (Tanga) pamoja na Sharp Striker (Korogwe).

Stori: Adam Mwanyakunga, Tanga

Leave A Reply