×

MSAMA YAFANYA OPERESHENI WANAODURUFU CD ZA WASANII

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex akishughulika na oparesheni hiyo.
Alex Msama akiwa amebeba vifaa vilivyokamatwa ambavyo vinatumika kurudufu kazi za wasanii
Askari wa jeshi la Polisi wakiwa na mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
Vijana wa kazi kutoka Msama Auction Mart wakipakia vyombo vinavyo tumika kurudufu kazi za wasanii kinyume cha Sheria.

 

 

KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni wasimamizi na wasambazaji wa kazi za Muziki wa Injili, chini ya Mkurugenzi wake, Alex Mwita Msama, imefanya oparesheni ya kuwakamata watu wanaodurufu CD feki za wasanii kupitia kompyuta walizokutwa nazo wakifanyia kazi hizo.

 

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya oparesheni hiyo iliyofanyika mitaa ya Kariakoo, Msama alisema kuwa, amekuwa akiwatahadharisha watu kuachana na kazi hiyo ya kudurufu CD feki, hivyo sasa kampuni yake imeanza zoezi hilo rasmi na sehemu nyingine nako wajiandae kupambana.

 

Alisema serikali inatengeneza mazingira safi na wafanyabiashara waaminifu wanaofuata utaratibu sahihi, ukiwemo ulipaji wa kodi kwa wakati na hivyo kampuni yake itaendelea kuhakikisha kazi za wasanii zinalindwa na kuheshimika ipasavyo.

 

Pia, katika kuonyesha msisitizo, Msama alisema; “Serikali ya awamu ya tano ni serikali ya kazi, hivyo haina chuki na mfanyabiashara yeyote anayefuata utaratibu wa kawaida ikiwemo kulipa kodi na mambo mengine ya kufanana na hayo.

 

“Nirudie tena wito wangu kwamba sasa biashara haramu ya kazi za wasanii basi na hii yote ni kutokana na kampeni yetu ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii na tutahakikisha tunawakamata wote watakaondelea na tabia hiyo.

 

“Tukiwaondoa wezi wa kazi za wasanii serikali itakusanya kodi halali. Kila mmoja awapige vita wachuuzi, wezi na maharamia wanaoiba kazi za sanaa kwa kuchoma CD feki. Kwa kufanya hivyo wananyonya jasho la wasanii na kuiingizia hasara serikali kwa kutolipa kodi halali.

 

“Sisi kama wasimamizi na wasambazaji wa kazi za sanaa tumeazimia kufanya ufuatiliaji kwa oparesheni maalum ambayo haina siku wala saa,” alisema Msama.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave a Comment