KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, anaiandaa safu yake ya ulinzi kuhakikisha hairuhusu bao katika mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya watani zao wa jadi Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, huku akisema ni kazi Omog ambaye yupo Zanzibar na kikosi chake cha Simba, anaifanya kazi hiyo kutokana na safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo kwa sasa inaongozwa na Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kuonekana kuwa hatari kwa timu pinzani.
Ajibu na Chirwa, mpaka sasa ndani ya kikosi cha Yanga wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao saba kati ya 10 ambayo timu hiyo imeyafunga msimu huu katika mechi saba.
Omog ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Nataka katika mchezo wetu dhidi ya Yanga tuweze kutoka uwanjani na ushindi safi ambao utakuwa na mabao kwa upande wetu lakini si kwa wapinzani.
“Najua ni kazi ngumu kumzuia mpinzani wako asifunge kutokana na kuwa na wachezaji mahiri, lakini tutajitahidi kuhakikisha hawafungi, lengo ni kupata pointi tatu dhidi yao na si kingine,” alisema Omog.
Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers
Android Bofya ===> Google Play
iOS Bofya ===>Apple Store
===
Stori: Omary Mdose | Championi Jumatano