×

Buswita: Nitawaonyesha Simba Kwa Nini Nimeichagua Yanga

AKITARAJIWA kucheza mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pius Buswita amesema atautumia mchezo ku­waonyeshea mashabiki wa timu hiyo kuwa haja­kosea kurudisha fedha za usajili za Simba ili atue Jangwani.

 

Kiungo huyo, hivi karibuni aliwekewa pingamizi na Simba katika usajili wake baada ya kusaini Yanga kwa kile kili­choelezwa kusaini klabu mbili tofauti kabla ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia hadi atakaporejesha shilingi milioni 10 alizozichukua kutoka Simba.

 

Nyota huyo, baadaye alirudi­sha fedha hizo na kurejea kuanza kucheza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Buswita alisema mechi ngumu ndizo anazozipenda kwa ajili ya kudhihirisha ubora wake alionao, hivyo ame­jiandaa vema ku­hakikisha anaonye­sha kiwango kikubwa katika mchezo huo.

 

Bus­wita al­isema, ana vitu vya kui­fanyia klabu yake ya Yanga ikiwemo kuifung­ia na kutengeneza nafasi za mabao kama shukrani baada ya kutua kuichezea timu hiyo katika msimu huu.

 

“Niliumia kuikosa mechi iliyopita dhidi ya Simba, kocha alinipanga katika kikosi cha kwanza alichoki­panga kianze, lakini dakika za mwishoni niliondolewa baada ya viongozi wa Simba kuniwekea pingamizi TFF baada ya kuchukua fedha zao za usajili na kunitaka nirudishe ndiyo nicheze.

 

“Hivyo, basi baada ya kuikosa mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, mechi hii ya ligi kuu ninaamini nitakuwepo kwenye kikosi kitaka­chocheza na Simba, hivyo ni mechi kubwa kwangu kucheza ambayo nimepanga kuonyesha ki­wango kikubwa.

“Nitacheza mechi hii kwa lengo la kuwaonyeshea Wanayanga kwa nini nilirudisha fedha za Simba ili niichezee Yanga ka­tika msimu huu ni­kitokea Mbao FC,” alisema Buswita ambaye amei­fungia Yanga bao moja katika mechi mbili ali­zozicheza.

Leave a Comment