×

SIMBA, YANGA: SOKABET NI HABARI NYINGINE KABISA MJINI, SOMA WALICHOKISEMA

Mtangazaji wa Global TV Online, Easter Msofe akizungumza na wadau mbalimbali wa Simba na Yanga maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa, mashabiki hao walikuwa wakitambiana kuhusu mchezo wa timu hizo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Jumamosi hii.

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba, presha imekuwa kubwa ambapo kila kona ya Jiji la Dar es Salaam gumzo ni mchezo huo wa wapinzani wa jadi.

 

Esther Msofe akiwafafanulia jambo mashabiki hao kuhusu Kampuni ya Sokabet ambao ndiyo waliodhamini kipindi hicho.

Timu hizo zinakutana zote zikiwa zimetoka kuweka kambi nje ya jiji, ambapo Simba wao walikuwa Unguja wakati Yanga wao walikuwa Morogoro na inavyoonekana kazi itakuwa ngumu kwenye Uwanja wa Uhuru ambapo mchezo huo utachezwa, kesho Jumamosi.

 

…mjadala ukiendelea.

Kituo cha runinga ya mtandaoni cha Global TV Online, leo Ijumaa kilirusha kipindi ambacho kilihusisha mashabiki wa pande hizo mbili chini ya udhamini wa Kampuni ya Sokabet na ‘povu’ lilimwagwa kwa wingi na mashabiki wa pande zote.

 

Shabiki wa Simba akifafanua kuhusu timu yake kuelekea mchezo huo.

Mtangazaji wa Global TV Online, Easter Msofe ndiye aliyeongoza kipindi hicho kwa kuzungumza na mashabiki wa maeneo tofauti ikiwemo Ubungo na Magomeni jijini Dar.

 

Shabiki wa Simba akijinadi kuwa timu yake itapata ushindi.

Kila upande ulikuwa ukivutia kwake kuhusu mchezo huo wa leo, ambapo wale wa Yanga wengi wao walionekana kuwa na imani na mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu na kiungo wao, Papy Tshishimbi na kudai kuwa wataongoza kuwamaliza Simba mapema.

 

Esther Msofe akiwagawia vipeperushi vya Sokabet mashabiki maeneo ya Magomeni.

Wale wa Simba wao walikuwa bize kujinadi kuwa Emmanuel Okwi atawalaza mapema Yanga kwa kuwa ni mzoefu na anawajua Yanga kwa kuwa amecheza nao mara nyingi.

Mashabiki wakimsikiliza kwa umakini Esther Msofe.

Mbali na hapo, mashabiki hao walijipatia zawadi ya fedha kiasi tofauti kutokana na kujibu maswali kuhusu wanavyoifahamu Kampuni ya Sokabet ambayo inajihusisha na masuala ya kubashiri matokeo.

Mjadala ukiendelea.

Baadhi ya mashabiki waliojipatia fedha ni Fumba Abdul Said na Nassor Meshack ambao walionyesha uhodari wa kufahamu jinsi Sokabet inavyofanya kazi ikiwemo na kutambua kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa Majimaji, timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mashabiki wakifurahia zawadi za fedha na fulana walizozawadiwa na mtangazaji Esther Msofe.

 VIDEO: SIMBA, YANGA: SOKABET NI HABARI NYINGINE KABISA MJINI

Leave a Comment