×

Dk 360 Zamkwamisha Pluijm Singida

Wachezaji wa Singida United.

LICHA ya kuwa na kikosi imara na washambuliaji wa kimataifa, bado Singida United imeshindwa kutamba katika michezo yake minne mfululizo kwa kutofunga bao lolote huku ikiwa na jumla ya mabao sita pekee
hadi sasa katika Ligi Kuu Bara.

 

Singida tayari imecheza michezo tisa mpaka sasa ikiwa na alama 14 ikiongozwa na Kocha Hans van Der Pluijm ambaye ameanza kuinoa msimu huu baada ya kupanda ligi kuu.

 

Kikosi hicho katika safu ya ushambuliaji kinaongozwa na Danny Usengimana, Michelle Katsvairo na Atupele Green ambao katika mechi tisa safu hii imetikisa nyavu mara sita tu na kuruhusu mabao manne tu.

 

Singida imeshindwa kupata ushindi katika michezo yake minne mfululizo dhidi ya Yanga, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Ruvu Shooting katika michezo yote hii walitoka sare ya bila kufungana. Ikumbukwe Singida inafundishwa na kocha mzoefu Pluijm ambaye amewahi kuipatia Yanga ubingwa na kutoa mfungaji bora katika kikosi hicho.

STORI: MARTHA MBOMA

Leave a Comment